Siku kadhaa baada ya Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) kuliandikia barua Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata) kufuatia sakata la mrundikano wa maombi ya msamaha wa kodi na manunuzi ya magari 82 ndani ya muda mfupi, Baraza hilo limechukua hatua.

Kupitia taarifa kwa vyombo vya habari, Mufti wa Tanzania, Sheikh Abu Bakari Zuberi ametangaza kumsimamisha kazi, Karim Majaliwa aliyekuwa Mkurugenzi wa Utawala wa Bakwata makao Makuu.

Mufti Zuberi ameeleza kuwa amemsimamisha Majaliwa kwa tuhuma za matumizi mabaya ya ofisi na kadhia ya magari 82 ili kupisha uchunguzi.

Aliongeza kuwa ameunda timu maalum kwa ajili ya kufanya maboresho ndani ya Bakwata ambapo itakuwa na jukumu la kupitia upya mikataba.

“Aidha timu hii nimeipa majukumu ya kukagua hesabu za BAKWATA kuanzia ngazi ya Makao Makuu na nchi nzima,” ilieleza taarifa hiyo ya Mufti.

Kikwete Ajibu Tuhuma Za Kulea Ufisadi Bandarini, Awapiga Kijembe Ukawa
Shule Binafsi Zatakiwa Kuwasilisha Ongezeko La Ada