Klabu ya Man City imepokea taarifa za kusikitishwa kutoka nchini Hispania, kufuatia kiungo  wao David Silva kuumia kifundo cha mguu alipokua kwenye majukumu ya timu ya taifa mwishoni mwa juma lililopita.

Silva aliumia katika mchezo wa kuwania kufuzu fainali za mataifa ya barani Ulaya, ambapo Hispania walikua na kibarua cha kuwakabili Luxembourg ambao walikubalia kichapo cha mabao manae kwa sifuri.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 29, aliumia mapema katika kipindi cha kwanza baada ya kukabiliwa vikali na kiungo wa Luxembourg, Lars Gerson.

Baada ya mchezo huo kocha mkuu wa timu ya taifa ya Hispania, Vicente del Bosque aliulizwa na waandishi wa habari, ni lini Silva anatarajia kurejea uwanjani, lakini hakua na jibu kamili ambalo lingetoa uhakika wa mchezaji huyo kuonekana mapema akiwa na wenziwe kwenye mapambano ya siku za hivi karibuni.

Tanzia: Abdallah Kigoda Afariki Dunia
Jurgen Klopp Aanza Mbwembwe