Kadhia ya upungufu wa sehemu bora za kujisitili (choo bora) katika baadhi ya maeneo ya vyuo vikuu jijini Dar es Salaam inayoambatana na ukosefu wa maji ya kutosha katika vyoo hivyo limepelekea baadhi ya wanafunzi hao kuingia gharama ya ziada.

Kwa mujibu wa taarifa iliyorushwa leo na BBC, baadhi ya wanafunzi wa vyuo vikuu jijini Dar es Salaam, hususan vilivyopo karibu na maeneo ya karibu na Maduka Makubwa hulazimika kufunga safari hadi kwenye maduka hayo kwa lengo la kijisitiri katika vyoo vya maduka hayo.

Mwanafunzi mmoja wa kike ambaye hakutaka jina lake litajwe alisema kuwa kutokana na upungufu wa mashimo ya choo na maji ya kutosha, wanafunzi hasa huwa katika hatari zaidi ya kupata magonjwa kama UTI, hivyo baadhi yao hufunga safari hadi ‘Mlimani City’ ili wapate huduma bora ya vyoo.

“Kwa upande wa akina dada, ukiona ile hali inazidi kuwa mbaya na maji labda hakuna, inabidi alazimike kusafiri kwenda Mlimani City ajisaidie huko ndio arudi huku campus,” alisema msichana huyo.

Naye mwanafunzi mwingine wa kiume alieleza kuwa hali huwa mbaya na kutishia kusambaa kwa magonjwa wakati maji yanapokosekana kwa muda mrefu katika maeneo ya vyuo yenye mkusanyiko wa watu wengi.

Madaktari Kumpandikizia Mwanajeshi Uume wa Marehemu
Filamu Ya Simba Na Hassan Kessy Yafungua Ukurasa Mpya