Mshambuliaji na nahodha kutoka nachini Wales, Gareth Bale amekanusha uvumi unaoendelea katika mitandao ya kijamii, kwamba hana maelewano mazuri na meneja wa sasa wa Real Madrid, Zinedine Zidane.

Bale amekanusha uvumi huo, kwa kusema maneno yanaendelea kuzungumzwa na kuandikwa hayana ukweli wowote, huku akiwataka mashabiki duniani kote kufuatilia namna ya ushirikishwaji wake kwenye kikosi tangu mfaransa huyo alipokabidhiwa timu.

Akihojiwa, mchezaji huyo wa zamani wa Spurs ya Uingereza amesema kwamba kabla kikosi hicho kukabidhiwa kwa Zidane, alikuwa na mpango wa kuondoka Madrid lakini sasa ameanza kufuta ndoto hizo.

“Kama ningeendelea kubaki mikononi mwa makocha waliopita, nadhani ningemaliza mkataba wangu na kuondoka, lakini sasa naanzxa kufuta mawazo hayo,” amesema na kuongeza:

“Ujio wa Zidane umenifanya niwe kma nilivyokuwa Spurs wakati ambao nilikuwa naaminiwa na kufunga mabao.

Wakati mwingine sisi tunakufa kimpira si kwasababu ya hiari yetu bali tunalazimishwa kufa kutokana na matakwa ya watu wengine.”

Mwanasoka huyo amesema kwamba anataka kuonyesha kwamba yeye ni muhimu katika kikosi cha Madrid lakini hataki kuwekwa benchi mara kwa mara na kumfanya ajutie kusaini katika kikosi cha matajiri hao.

“Unaposajiliwa kwenye klabu kubwa kama hii ni lazima ukutane na watu wengine wenye majina makubwa lakini lazima wale waliokusajili wajue kwamba kama usingekuwa mkubwa, pia usingesajiliwa, ni lazima wakupe nafasi ya kuonyesha ukubwa wako,” amesema.

Meneja aliyepita wa Real Madrid, Rafael Benitez amekuwa na misimamo yake kiasi kwamba hakuwa anamtumia sana Bale lakini sasa baada ya zidane kupewa mikoba yake, mwanasoka huyo ameanza kuwa na furaha katika maisha ya kikosi hicho.

Muelekeo Wa Upepo Wa Samatta Wageuka Akiwa Lubumbashi
Jurgen Klopp Awatuliza Mashabiki Wa Liverpool