Mshambuliaji wa pembeni wa klabu ya Real Madrid, Gareth Bale usiku wa kuamkia hii leo alitangazwa kuwa mchezaji bora wa mwaka kupitia chama cha soka nchini Wales (FAW).

Bale ametangaza kuwa mshindi wa tuzo hiyo, ikiwa ni mara yake ya tano.

Bale pia ametangazwa kuwa mchezaji bora wa tuzo ya mashabiki na wachezaji wa soka nchini Wales ambayo huambatana na ile ya chama cha soka.

Kura zilizopigwa zimeonyesha Bale, aliwashinda wenzake kwa mbali kutokana na juhudi alizozionyesha akiwa na klabu yake ya Real Madrid, sambamba na kuisaidia timu yake ya taifa ambayo inahitaji point moja ili ijihakikishie nafasi ya kucheza fainali za kombe la Ulaya za mwaka 2016.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 26, alifunga bao pekee lililoipa ushindi Wales dhidi ya Ubelgiji mwezi June na pia alifunga tena katika mchezo dhidi ya Cyprus walioloweshwa kwa bao moja mwezi septemba na kuibua matarajio chanya ya kucheza fainali za Ulaya.

Tuzo zilizotolewa usiku wa kuakia hii leo katika hafla ya chama cha soka nchini Wales upande wa wanaume:

Mchezaji bora wa mwaka: Gareth Bale

Mchezaji bora wa mwaka kwa kura za wachezaji: Gareth Bale

Mchezaji bora wa mwaka kwa kura za mashabiki: Gareth Bale

Mchezaji bora wa mwaka mwenye umri mdogo: Tommy O’Sullivan

Chaguo la vyombo vya habari: Chris Coleman

Tuzo ya heshima ya FAW: Alan Curtis ambaye ni mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya Wales kati ya mwaka 1976–1987.

Mchezaji bora wa ligi ya nchini Wales: Sion Edwards (Bangor City FC)

Tuzo upande wa wanawake:

Mchezaji bora wa mwaka: Kylie Davies

Mchezaji bora wa mwaka kwa kura za wachezaji: Helen Ward

Mchezaji bora wa mwaka kwa kura za mashabiki: Natasha Harding

Mchezaji bora wa mwaka mwenye umri mdogo: Charlie Estcourt

Rodgers Aondoka Kwa Kuacha ujumbe Mzito
‘Na Uhakika, CCM Itashinda Uchaguzi Mkuu’