Mshambuliaji wa zamani wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Young Africans Boniface Ambani amesema kiwango kinachoonyeshwa na Mshambuliaji wa Simba SC, Jean Baleke kimeongeza presha ya mchezo wa Dabi.

Simba SC itakutana na Young Africans katika mchezo wa Mzunguuko wa 26 wa Ligi Kuu Tanzania Bara kesho Jumapili (April 16) katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam, kuanzia saa 11 jioni.

Akizungumza kutoka Kenya, Ambani amesema mashabiki wa Young Africans walikuwa wanajiamini katika mchezo huo ingawa kiwango cha Baleke kimerudisha matumaini Simba SC, kuamini pia wanaweza kushinda.

“Mchezo wa Dabi hautabiriki na hauangalii kiwango cha timu katika muda husika isipokuwa ni kwa jinsi gani wachezaji wa timu zote wameandaliwa vizuri kimbinu, kisaikolojia na kiakili,” amesema Ambani

Ambani aliongeza kuwa moja ya Dabi ambayo hataisahau ni ile ya mwaka 2008 ambayo waliifunga Simba bao 1-0.

“Nakumbuka nilitoa pasi ya bao kwa Benard Mwalala na kuvunja uteja baada ya kutoifunga Simba kwa misimu minane, pia na uwezo mkubwa niliouonyesha tofauti na matarajio ya wengi,” amesema.

Tangu Baleke ajiunge na Simba dirisha dogo la Januari mwaka huu akitokea Nejmeh ya Lebanon kwa mkopo akitoka TP Mazembe, amekuwa tegemeo kwani hadi sasa amefunga mabao saba ya Ligi Kuu Bara.

Kisa Mane, Leroy Sane aupigia magoti Uongozi
Vinicius Junior: Ancelotti anafaa kuinoa Brazil