Mshambuliaji Super Mario Balotelli, usiku wa kuamkia hii leo alifunga bao la kwanza akiwa na klabu ya AC Milan, tangu aliposajiliwa kwa mkopo mwezi uliopita akitokea Liverpool nchini England.

Balotelli alifunga bao la kwanza miongoni mwa mabao matatu ya AC Milan katika mchezo dhidi ya Udinise waliopata mabao mawili ya kujipoza machungu.

Balotelli, aliyerejea klabuni hapo kwa mkopo, alifunga bao hilo katika dakika ya 6, kwa mpira wa adhabu ndogo ambao ulikwenda moja kwa moja kwenye lango la timu mwenyeji.

Mabao mengine ya AC Milan katika mchezo ho yalifungwana Giacomo Bonaventura pamoja na Cristian Zapata katika dakika ya 10 na 45 .

Mabao ya wenyeji yalifungwa na Emmanuel Badu na Duvan Zapata katika dakika ya 51 na 58.

Kufunga bao kwa Balotelli kumewafurahisha wachezaji pamoja na mashabiki wa AC Milan ambao walikua wakisubiri kumuona mshambuliaji huyo akiwa kwenye furaha ya kuiwezesha ushindi klabu hiyo.

Mmoja wa wachezaji waliodhihirisha furaha hadharani ni kiungo kutoka nchini Uholanzi Nigel De Jong, ambaye alionekana akimshurutisha Balotelli kushangili bao alilolifunga, lakini ilikua tofauti na alivyotaka.

Balotelli alikua na wakati mgumu wa kuonyesha kiwango chake akiwa na Liverpool waliyomsajili mwanzoni mwa msimu uliopita na wakati mwingine alishindwa kufunga mabao kama alivyokua anatarajiwa na mashabiki wengi wa klabu hiyo, hali ambayo ilionekana kumsononesha hadi kufikia hatua ya kushindwa kujihakikishia nafasi kwenye kikosi cha kwanza.

Zitto Kabwe Awatumia Ujumbe Twaweza
CCM Yataja Idadi Ya Simu Alizonazo Magufuli Kama Sifa Ya Rais Anayefaa!