Mshambuliaji kutoka nchini Italia Super Mario Balotelli Barwuah amekamilisha taratibu za kusajiliw ana klabu ya AC Monza, inayocheza Ligi daraja la pili nchini humo (Serie B).

Balotelli amesajiliwa na klabu hiyo akiwa mchezaji huru, baada ya kukatisha mkataba wake na klabu ya Brescia, ambayo ilishuka daraja msimu uliopita, ikitokea Ligi Kuu (Sirie A) hadi ligi daraja la pili (Sirie B).

Sababu kubwa ya mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 30 kukatisha mkataba wake na klabu ya Brescia, ni baada ya kutohudhuria mazoezi na timu hiyo kwa mwezi Juni na Julai, pasina na kutoa udhuru wowote.

Balotelli aliyewahi kucheza kwenye Ligi Kuu ya England akiwa na klabu za Liverpool na Manchester City, amekua na rekodi mbaya ya utukutu, hali ainayomfanya ashindwe kudumu kwenye klabu moja kwa muda mrefu.

Balotelli baada ya kukamilisha usajili wa kujiunga na AC Monza

Hata hivyo ana rekodi ya kutwaa taji la England (EPL) akiwa na Man City (2012) na kwa upande wa nchini kwao Italia, alitwaa taji la Serie A mara tatu akiwa na Inter Millan.

Klabu nyingine alizowahi kuzitumikia ni Lumezzane (2006–2007), Inter Milan (2007–2010), Manchester City (2010–2013),  AC Milan (2013–2014/ 2015–2016 Mkopo), Liverpool (2014–2016), Nice (2016–2019), Olympic Marseille (2019) na Brescia (2019–2020).

Ozil anukia Uturuki, rafiki yake aanika ukweli wote
Azam FC kujipanga upya VPL, wapata alama mbili kanda ya ziwa

Comments

comments