Mshambuliaji wa klabu ya Liverpool Super Mario Balotelli, ameonyesha msimamo wa kutokua tayari kurejea nyumbani kwao Italia kujiunga na klabu ya Sampdoria, na badala yake anahitaji kuelekea nchini Hispania kuitumikia klabu ya Sevilla.

Watu wa karibu wa mshambuliaji huyo, wamevieleza baadhi ya vyombo vya habari nchini Italia kwamba, Balotelli hayupo tayari kurejea katika ligi ya Serie A, na anahitaji kupata changamoto mpya kwenye ligi ya nchini Hispania.

Uongozi wa klabu ya Sampdoria tayari umeshaonyesha nia ya dhati ya kumsajili Balotelli baada ya Liverpool kumuweka sokoni katika kipindi hiki cha majira ya kiangazi, lakini mpango huo umekua ukikwamishwa na muhusika ambaye alitakiwa kukaa meza na viongozi wa il Doria ili kukubaliana maslahi binafsi.

Balotelli amepoteza nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza cha Liverpool, tangu msimu uliopita na mambo yaliendelea kuwa magumu kwake baada ya kusajiliwa kwa mshambuliaji kutoka nchini Ubelgiji Christian Benteke Liolo.

Azam FC: Suala La Muamuzi Sio Kazi Yetu
Diamond Akamilisha Collabo Na Ne-Yo, Aitabiria Mema