Aliyekuwa Balozi wa Tanzania Nchini Urusi wakati huo, Patrick Chokala amefichua siri jinsi walivyomsafirisha kijasusi ‘Bilionea’ wa nyumba za Lugumi Dkt. Louis Shika kurudi nyumbani Tanzania.

Chokala aliyekuwa nchini Uriusi miaka ya 2002 mpaka na 2008 katika kipindi ambacho sakata la utekwaji wa Dkt. Shika lilijitokeza, amethibitisha kuwa ni kweli Mtanzania huyo kuwa ni daktari na kwamba aliwahi kutekwa.

Dkt. Shika anatuhumiwa kuvuruga mnada wa Majumba ya mfanyabiashara maarufu, Saidi Lugumi uliofanywa na Kampuni ya Yono baada ya kufika bei ya kuzinunua nyumba hizo tatu kwa sh. 3.2 bilioni, lakini akashindwa kutimiza sharti la kulipa asilimia 25 ya fedha hizo.

Aidha, Balozi Chokala amesema kuwa anakumbuka tukio la Dkt. Shika la kutekwa na majambazi kutokana majigambo yake kuwa anapesa nyingi na kuwashawishi watekaji hao kumfuatilia.

“Majigambo ya kumiliki fedha nyingi hayajaanza leo, kwani hata alipokuwa Urusi alikuwa anasema anamiliki fedha nyingi, watu walimuamini kwakuwa alikuwa daktari anayefahamika, matokeo ya majigambo yake yalipelekea kutekwa,”amesema Balozi Chokala

Hata hivyo, Balozi Chokala ameongeza kuwa baada ya Dkt. Shika kufanikiwa kuwatoroka watekaji akiwa amekatwa vidole kadhaa vya mikono yake, aliperlekwa hospitali huku ubalozi ukifanya mpango wa kusafirisha bila yeye kufahamu.

 

Tanzania bara yapangwa na Zanzibar CECAFA Challenge Cup 2017
Utovu wa nidhamu wamponza Aubameyang