Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge ametembelea Ubalozi wa Tanzania nchini Ethiopia kwa lengo la kujionea utendaji kazi wa Ubalozi pamoja na kukagua mali za Serikali nchini humo.

“Nawasihi sana kuacha kufanya kazi kwa mazoea na badala yake tufanye kazi kwa bidii na kuwa wabunifu wa kuitangaza Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,” Amesema Balozi Ibuge

Balozi Ibuge kabla ya kuanza kukagua mali za Serikali, alikutana na watumishi katika mkutano ambapo amewataka kufanya kazi kwa bidii, weledi na uaminifu kwa kuweka mbele maslahi ya Taifa.

Aidha Balozi Ibuge amekagua mali mbalimbali zinazomilikiwa na Serikali ya Tanzania nchini Ethiopia kwa lengo la kuijionea na kujiridhisha juu ya uwepo wa mali hizo.

Ubalozi wa Tanzania nchini Ethiopia unaiwakilisha Tanzania pia katika nchi za Djibouti, Yemen pamoja na Umoja wa Afrika na kamisheni ya Umoja wa Mataifa inayosimamia masuala ya Uchumi Barani Afrika (UNECA)..

Biden aandika historia nyingine Marekani
DFB kumpa ushirikiano Joachim Low