Katibu Mkuu  Kiongozi, Balozi John Kijazi amewataka wahandisi nchini kujipanga kutumia fursa ya uchumi wa viwanda katika maendeleo yao na ya Taifa kwa ujumla.

Balozi Kijazi ameyasema hayo katika Mkutano Mkuu wa 17 wa Wahandisi unaofanyika leo na kesho jijini Dodoma, ambao uliojadili mambo mbalimbali kuhusu sekta taaluma yao pamoja na kutoa mapendekezo yatakayopelekwa serikalini.

Amesema uchumi wa kati uliopatikana  hivi karibuni umechangiwa kwa kiasi kikubwa na wahandisi wa hapa nchini kwani miradi yote imekuwa ikifanywa na wao.

“Huu ndio wakati wa wahandisi kuonesha uwezo wao kwa vitendo kwani miradi yote inayofanyika hapa nchini inategemea wahandisi. Hivyo jipangeni, huu ni wakati wa Uchumi wa Viwanda”, amesema Kijazi.

“Serikali inaendelea kuboresha vyuo vinavyozalisha wahandisi hapa nchini kwa kuongeza majengo katika vyuo hivi ili kuondoa uhaba wa madarasa” ameongeza.

Katika mkutano huo jumla ya wahandisi 452 walipata kiapo mbele ya hakimu mfawidhi, huku wakikiri kulinda na kutekeleza miiko ya sheria na taratibu za uhandisi.

Lissu aahidi kuibadili Arusha, ‘Geneva ya Afrika’
KMC FC: Tupo tayari kwa Ligi Kuu 2020/21