Balozi wa Kenya nchini Tanzania Dan Kazungu ametoa wito kwa wananchi wa nchi hizo mbili kuhakikisha mlipuko wa virusi vya corona hauyumbishi mahusioano yaliyopo baina yao hasa ya kibiashara.

Balozi huyo ametoa wito huo mapema leo Mei 19 alipokuwa anaongea na waandishi wa habari juu ya sintofahamu ambayo imejitokeza baada ya mipaka inayounganisha nchi hizo kufungwa kutokana na virusi vya Corona.

Amesema tayari ameshaongea na viongozi amabo ni mawaziri wenye dhamana juu ya kujadili suluhisho na kwamba wao hawajazuia magari ya mizigo kuingia nchini kwao kwa madareva wakataofuata taratibu.

“sisi tunawaombea watanzania katika kupigana na janga hili, tuombeeni pia kule tupigane na jangahili, jangahili likikaa kando tuje pamoja na kufanya kazi” Amesema Kazungu

Aidha amebainisha kuwa huu sio muda muafaka wa watu kuanza kufarakanishwa na cororna bali ni muda wa kukaa na kupanga biashara zitafanyikaje baada ya janga hili kupita ili kuinua uchumi.

” tujiangalie je, baada ya kurona tunaweza kuja namna gani pamoja tufufue na kuendeleza zaidi uchumi wetu…mataifa mengine yanapanga” amesisitiza balozi huyo

Kisongo: Ndemla hana washauri wazuri
Miaka sitini jela kwa kubaka mwanafunzi