Maofisa waandamizi wa Jeshi la Polisi wametakiwa kuwa makini na uwasilishwaji wa taarifa kwa umma ili kuepuka baadhi ya watu wengine kuzibadilisha taarifa kwa lengo la kupotosha wananchi wakati wa majanga na dharura.

Hayo yamesemwa na Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, David Concar leo October 22, 2022 wakati akufunga mafunzo ya awamu ya pili ya kuwajengea uwezo wa mawasiliano maafisa wa Jeshi hilo wakati wa majanga na dharura.

Naye Kamishina wa intelijensia ya makosa ya Jinai CP Charles Mkumbo, amewataka washiriki kutumia mafuzo hayo vizuri kwa kutoa taarifa zinazozingatia vigezo ili kuepuka kutoa taarifa za upotosha katika jamii.

CP Mkumbo Pia amewashukuru wafadhiri wa mafunzo hayo kutoka ubalozi wa Uingereza, taasisi ya Mercy Corps pamoja na wawezeshaji kutoka chuo kikuu Dar es salaam kwa kutoa mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kupambana na majanga ya dharura pindi yanapotokea.

Askari 300 wapelekwa kuudhibiti moto mlima Kilimanjaro
Waandishi wa habari watakiwa kujua sheria