Imefahamika kuwa Uongozi wa Simba SC bado haujamalizana na wachezaji wake wawili walioomba kuondoka kikosini hapo, winga Mmalawi, Peter Banda na Mkenya Joash Onyango.

Simba SC ilipanga mwanzo kumtoa Banda kwa mkopo katika moja ya timu za Ligi Kuu, lakini inaelezwa nyota huyo machachari aligoma na kutaka alipwe fedha aondoke, jambo ambalo hadi sasa mabingwa hao zamani wanalitafutia ufumbuzi.

Kwa upande wa Onyango aliomba kuondoka Simba SC kutokana na kutokuwa na furaha, pia kutotimiziwa baadhi ya matakwa yake, lakini ni kama bado mabosi wa timu hiyo wanasita kumuachia wakihofia kukosa mbadala wake.

Hata hivyo, kama Simba SC itakamilisha usajili wa Caique, Onana, Malone, Aubin na Fabrice Ngoma, itahitaji kupunguza wachezaji wawili wa kigeni ili wabaki 12 kama taratibu zinavyotaka.

Kwa sasa, licha ya kutembeza ‘Thank You’ kwa baadhi ya wachezaji wake wa kigeni, Simba SC imebaki na maproo tisa ambao ni Jean Baleke, Saidi Ntibazonkiza, Clatous Chama, Banda, Pape Sakho, Moses Phiri, Onyango, Sadio Kanoute, na Henock Inonga, jambo linaloendelea kuwaumiza vichwa viongozi wamtoe nani licha ya kwamba Banda na Onyango wameonesha nia ya kuondoka.

“Usajili unaendelea na tutashusha majembe ya maana, lakini kuhusu hilo la Banda na Onyango bado hatujafika mwisho naomba tuachane nalo likitimia nitakujuza,” amesema kiongozi wa Simba SC.

Hadi sasa, Simba SC imeachana na Beno Kakolanya, Gadiel Michael, Mohamed Quattara, Ismael Sawadogo, Victor Akpan, Nelson Okwa, Jonas Mkude, Erasto Nyoni na Augustine Okrah.

Mifumo uchakataji takwimu kuepusha makisio huduma ya Dawa
Wananchi wapewa nguvu ujenzi kituo cha Afya