Waziri wa Ujenzi, Makame Mbarawa amesema Serikali imesisitiza kuwa Bandari ya Tanga haipo kwenye Mpango wa kuwekwa wawekezaji wa ndani au nje hivyo Wananchi wasiwe na wasiwasi.
Waziri Mbarawa aliyasema hayoWaziri Mbarawa ameyasema hayo wakati akizungumza na Watumishi wa Menejimenti ya Wizara ya Ujenzi na Menejimenti za Taasisi za Wizara hiyo kwenye kikao kazi cha siku tatu kilichofanyika mkoani Tanga.
Amesema “Bandari ya Tanga haipo kwenye Mpango wa kutafutiwa mwekezaji kwakuwa Haina changamoto,tulichokifanya nikuifanyia maboresho makubwa na tutaleta mitambo mingine ya kisasa zaidi ili iwe na ufanisi mkubwa zaidi ya hapa kwahiyo Wananchi wasiwe na wasiwasi juu ya hilo.”
Kauli hiyo, inakuja kufuatia gumzo la Bandari ya Dar es Salaam huku wakazi wa Tanga wakihoji hatma ya Bandari baada ya kufanyiwa maboresho ikiwamo uchimbaji wa kina Cha Bahari, Ujenzi wa magati pamoja na ununuzi wa mitambo ya kisasa ya upakua na upakiaji wa mizigo.
Aidha, Waziri Mbarawa pia aliwatahadharisha Watumishi wa Umma kuzingatia Maadili ya kazi zao na kujiepusha na vitendo visivyofaa ikiwamo uvujishaji wa Siri za Serikali nakwamba wote waliohusika na Uvujishaji wa Siri za Serikali watatafutwa na kuchukulia hatua huku akionekana kushangaa mkataba huo kusambazwa Sasa hivi Wakati ni wamuda mrefu.