Baada ya kukamilisjha usajili wa Kiungo kutoka DR Congo, Yanick Bangala akitokea Young Africans, uongozi wa kikosi cha Azam FC umechimba mkwara mzito kuwa msimu ujao hesabu yao kubwa ni ubingwa.

Azam FC juzi Jumamosi (Julai 29) walitoa taarifa rasmi ya kumalizana na Young Africans na kukamilisha usajili wa Bangala ambaye amesaini mkataba wa miaka miwili.

Bangala anakuwa staa wa pili kutoka Young Africans kujiunga na Azam FC kuelekea msimu ujao wa 2023/24, hii ni mara baada ya mapema kabisa kumalizana na Young Africans kwa kumsajili kiungo wa kimataifa wa Tanzania, Feisal Salum ‘Fei Toto’.

Akizungumza jijini Dar es salaam, Afisa Habari wa Azam, Hasheem Ibwe amesema: “Usajili mkubwa ambao umefanyika kupitia dirisha hili kubwa la usajili ni wazi unathibitisha kuwa kikosi chetu kina malengo makubwa msimu ujao.

“Kwa misimu kadhaa tumekuwa washindania ubingwa na kuishia kumaliza kwenye nafasi ya tatu, lakini msimu ujao tumejipanga kuhakikisha ubingwa unakuja Chamazi baada ya miaka mingi kupita. Kutokana na ubora wa kikosi tulichonacho tunaamini hili linawezekana.”

Chama: Onana atafunga sana Ligi Kuu
Wakulima ongezeni thamani ya zao la Alizeti - COSITA