Naibu Gavanna wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) Dkt. Bernard Kibesse amezindua muunganiko wa benki tatu zilizounda benki moja inayojulikana kama ‘Mwanga Hakika Microfiance Bank Ltd’ yenye mali ya thamani ya shilingi bilioni 40.5, amesema muunganiko huo utasaidia ukuaji wa uchumi itakuwa na wigo mpana wa kutoa mikopo.

Naibu Gavana wa BoT, Dkt kibesse amepongeza hatua iliyochukuliwa na benki hizo na kwamba itasaidia katika uimarishaji wa sekta ya kibenki kwa kuhakikisha watu ambao hawajafikiwa na huduma wanapata nafasi hiyo.

Pia, amesema itasaidia katika kuchochea ukuaji wa uchumi kwani benki hiyo itakuwa na wigo mpana wa kutoa mikopo hasa kwa wajasiriamali wadogo na wa kati jambo litakalochangia kuleta ujumuishwaji wa uchumi.

“Sekta ya kibenki ni muhimu katika kuchangia maendeleo ya taifa kupitia ajira na kuchochea ukuaji wa biashara ndogo na za kati kupitia mikopo nafuu.Tunaamini kwamba benki hii itachangia katika uimarishaji wa sekta hii na hatimaye kuongeza ujumuishwaji wa watu kiuchumi hapa nchini,”amesema Dkt.Kibesse.

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa benki hiyo, Eng. Ridhuan Mringo alisema muungano huo ni muhimu katika kuunda benki imara inayoweza kutoa huduma zenye viwango kwa wateja zenye kuzingatia unafuu na teknolojia za kisasa.

Muunganiko huo umefanikiwa kufuatia uthibitisho kutoka benki ya Tanzania (BoT) pamoja na Tume ya ushindani (FCC) na kupelekea kuundwa kwa Benki moja yenye  thamani ya 40.5 bilioni ya mali.Pia, benki hiyo inatarajia kuongeza nguvu ya ushindani katika soko nchini.

Ujenzi SGR wakamilika 87%
Tanzania yaneemeka saruji kupata soko nje