Utafiti uliofanywa na chuo kikuu cha McGill nchini Canada mapema mwezi huu umeonyesha ongezeko kubwa la kina mama  kulea familia zao wenyewe.

Katika utafiti huo kina mama wengi walisema kwamba kulea familia pekee haina ubaya wowote ili mradi familia iwe na furaha wakitolea mfano ya baadhi ya watu maafuru walilelewa na mzazi mmoja kama vile rais wa Marekani Barack Obama, mcheza filamu Jet Li, na baadhi ya wasanii wa mziki kama vile Kanye West, Jay Z, Mariah Carey, Angelina jolie, Diamond Platinumz.

Utafuti huo pia ulionesha sababu mbalimbali zinazopelekea watoto wengi kulelewa na mzazi mmoja haswa mama, ukiachana na sababu ya kifo sababu nyingine ni mimba zisizo tarajiwa, vijana/baba wengi kukosa ushirikiano kutokana na kukosa  utayari wa kubeba jukumu la malezi.  Mimba nyingi zinazopatikana nje ya ndoa hupelekea mtoto kupata malezi ya mzazi mmoja yaani single parent

Kwa watu wengine malezi ya mzazi mmoja husababishwa na ugumu wa kupata mchumba kwani siku hizi kuna tatizo moja, vijana wanakuwa na shughuli nyingi kiasi kwamba, suala hilo wanaliweka kando kwanza. Wanajitahidi kuhakikisha wanajiweka vizuri kiuchumi, kwamba ana nyumba, gari, na akiba ya kutosha, ndipo sasa anaanza kutafuta mchumba.

Na mpaka hayo yote yatimie, muda unakuwa umekwenda, umri nao umesogea, hajui hata pa kuanzia. Ndio maana katika nchi nyingine kuna zile tovuti zinazotumiwa kutafutia watu wachumba. Maana mwisho wa siku mtu anaona afadhali apeleke maelezo yake na picha kwenye tovuti hizo ambazo zitamtafutia mwanaume au mwanamke ambaye wanaendana, kisha kuwakutanisha pamoja.

 

 

 

Moutinho Aeleza Alivyoshindwa Kujiunga Na Spurs
David Moyes Aufyata, Kufanya Kazi Na Lamine Kone