Baraka Da Prince amedai kushtukia ‘mchezo mchafu’ unaofanywa kwenye akaunti yake ya YouTube ili video ya wimbo wake mpya ‘Sometimes’ isipate watazamaji wengi.

Mkali huyo kutoka Jiji la Miamba, Mwanza amesema amebaini mchezo huo baada ya kupata taarifa kuwa kuna baadhi ya nchi mashabiki wake wanashindwa kuitazama video hiyo, huku video za wasanii wengine wa Tanzania zikionekana kama kawaida.

“Kuna mchezo mchafu unafanyika kwenye YouTube yangu. Unaweza ukashangaa video yangu inafika labda views 20,000, lakini baada ya masaa mawili inarudi views 18,000,” Baraka aliiambia The Playlist ya Times FM.

“Ina maana kuna kitu kinafanyika kwenye YouTube yangu na yote ili kunifelisha mipango yangu ionekane namba yangu imeshuka. Fan base yangu mimi nashukuru imerudi vizuri,” alifunguka.

 

Barakah ambaye alijiengua kwenye lebo ya RockStar 4000 miezi kadhaa iliyopita, amekuwa akizing’arisha nyimbo za wasanii wa muziki wa hip hop kama OMG (Uongo na Umbea), Bonta (Tokomeza Zero), Moni (Matango Pori).

Wachina 9 wanyang'anywa hati za kusafiria
Video: Nyalandu atunisha misuli, CCM yaionya Chadema