Wamiliki wa baa wametakiwa kuhakikisha wahudumu wao wote wanavaa barakoa kwaajili ya kujikinga na kuzuia maambukizi ya virusi vya covid 19.
Hayo yamebainishwa na mkuu wa wilaya ya Iringa, Richard Kasesela alipozungumza na wamiliki wa baa na kusisitiza kuwa ni muhimu kwa wahudumu hao pia kunawa mikono kwa maji tiba.
Mbali na wahudumu wa baa amewataka wamiliki wa sehemu zenye mikusanyiko ya watu kuhakikisha kuna maji yanayotiririka na sabuni kama wizara ya afya ilivyoelekeza.
Magufuli atuma rambirambi vifo ajali ya Mkuranga
Halikadharika mkuu huyo wa wilaya amewataka wamiliki kuhakikisha wateja wanakaa umbali wa kuanzia mita moja baina ya mtu mmoja na mwingine ili kujikinga na maambukizi.
” Wale wote anaokuwa kwenye maeneo ya burudani wanapaswa kukaa umbali unaotakiwa na watakaokiuka watachukuliwa hatua kwa kufunga biashara zao” Amsema DC Kasesela.
Aidha amesema kuhusu muda wa kufunga baa, manispaa hiyo itaangalia muda wa kufunga kwakuwa wapo wanaoendelea kufanya biashara hadi usiku wa manene.