Baraza la kijeshi linalotawala nchini Sudan limekiri kwamba vikosi vya usalama vilikiuka sheria wakati wa kuwatawanya waandamanaji nje ya makao makuu ya jeshi katika mji mkuu wa nchi hiyo Khartoum wiki iliyopita.
Msemaji wa baraza hilo la mpito, Jenerali Shamseddin Kabashi, amekiri kuwa vikosi vya jeshi vilikiuka sheria kwa kuwashambulia waandamanaji hao, hivyo uchunguzi bado unaendelea na kwamba maafisa kadhaa wa kijeshi wamewekwa kizuizini kwa madai ya kukiuka maelekezo ya viongozi wa kijeshi lakini jenerali Kabashi hakufafanua zaidi.
Hata hivyo, kulingana na waandaaji wa maandamano hayo ya Sudan, wamesema kuwa takribani watu wapatao 100 waliuawa katika mji mkuu wa Khartoum wakati wa makabiliano na vikosi vya usalama, huku waandamanaji wakisema kuwa zaidi ya miili 40 iliopolewa katika Mto Nile.