Afisa Mtendaji Mkuu wa Simba SC Barbara Gonzalez ameanika mipango na mikakati ya usajili kuelekea mwishoni mwa msimu huu, tayari kwa msimu ujao wa Ligi Kuu na Michuano ya Kimataifa.
Hatua hiyo ya Bodi ya Wakurugenzi Simba Sc imekuja kufuatia mwenendo wa Kikosi cha klabu hiyo kushindwa kufikia lengo la kutetea Ubingwa wa Tanzania bara pamoja na kufika Nusu Fainali Kombe la Shirikisho Barani Afrika.
Imebainika wazi kuwa Safu ya Ushambuliaji ndio tatizo kubwa hadi kushindwa kufikiwa kwa malengo hayo, hivyo Bodi hiyo imejipanga kurudisha makali kwa kuteua kamati ndogo ya usajili ambayo itaifanyia kazi Ripoti ya Kocha Franco Pablo Martin itakayowasilishwa mwishoni mwa msimu huu.
“Akili zetu kwa sasa ni namna ambavyo tunaumaliza msimu, tunalihitaji zaidi Kombe la Shirikisho Tanzania Bara ‘ASFC’ ili libaki kwetu, najua inawezekana kwa sababu kocha wetu anatambua hilo wachezaji nao wanalitambua hilo,”
“Kuhusu hilo suala la usajili ni kweli, wakati ni sasa ni kwambie tu, watu wapo kazini tayari, Rais wa Heshima Mohamed Dewji ametuhakikishia hakuna mchezaji kocha atamtaka asije Simba SC.”
“Tunakwenda kufanya usajili Bora ambao huenda haijawahi kutokea, wanasimba furaha yao itarejea kwa kiwango kikubwa, viongozi wao tuko makini.” Amesema Barabara Gonzalez.
Ahmed Ally: Hatujasahau machungu ya Bukoba
Wachezaji wanaodaiwa kuwindwa na Simba SC ni Mshambuliaji wa US Gendamarie Victorian Adebayor raia wa Niger, Mshambuliaji wa Zanaco FC Moses Phiri raia wa Zambia, Kiungo Mshambuliaji wa klabu ya ASEC Mimosas ya Ivory Coast Stephan Aziz Ki raia wa Boukina Fasso na Kiungo kutoka DR Congo Zemanga Soze anayeitumikia klabu ya TP Mazembe.