Rais wa Barcelona, Joan Laporta yupo tayari kupitisha panga kwenye kikosi cha kwanza cha miamba hiyo ya Nou Camp kusafisha wachezaji wasiohitajika na kuleta wengine wapya kupiga kazi.

Antoine Griezmann na Philippe Coutinho ni miongoni mwa mastaa wanaotajwa wanaweza kuwamo kwenye orodha hiyo ya watakaopigwa bei dirisha lijalo la uhamisho wa majira ya kiangazi.

Wachezaji wengine wanaotajwa huenda wakaondoka ni Ousmane Dembele, Coutinho, Miralem Pjanic, Martin Braithwaite, Junior Firpo na Neto.

Beki wa kati, Samuel Umtiti naye anaweza akaondoka kutokana na kusumbuliwa na majeruhi ya mara kwa mara. Matheus Fernandes naye yupo kwenye orodha ya watakaouzwa huku Riqui Puig akijiandaa kutoka kwa mkopo.

Wachezaji kama Francisco Trincao, Sergino Dest na Clement Lenglet bado hatima zao hazipo wazi, lakini kama Kocha Ronald Koeman atapata wachezaji sahihi wa kuziba mapengo yao, ataruhusu waondoke.

Kwa wakati huu, wachezaji Gerard Pique, Jordi Alba, Sergio Busquets na Sergi Roberto wameripotiwa kuwa salama, huku wachezaji ambao hawataguswa kabisa ni Messi, Frenkie de Jong, Marc-Andre ter Stegen, Ronald Araujo, Oscar Mingueza, Pedri, Ilaix Moriba na Ansu Fati.

Serikali: Kilimo cha bangi hapana!
Kiongozi wa mapinduzi ya Mali ajitangaza Rais, awavua madaraka Rais, Waziri Mkuu