Klabu ya Barcelona imemteua mchezaji wa zamani wa klabu hiyo Eric Abidal kuwa mkurugenzi mpya wa michezo kwa msimu wa mwaka 2018-2019 akichukuwa nafasi ya Robert Fernandez ambaye alikuwa akiitumikia nafasi hiyo.
Abidal anarajia kuanza rasmi kazi yake kama mkurugenzi mpya wa michezo wa Barcelona tarehe 18 mwezi Julai. Mchezaji huyo aliwahi kuichezea klabu ya Barcelona katika miaka ya 2007 hadi 2013 kabla yakukumbwa na ugonjwa mkubwa katika Ini lake, ambapo ilimbidi kufanyiwa upasuaji.
Uongozi wa Barcelona umefikia uamuzi wa kumteua Eric Abidal kutokana Mkataba wa Robert Fernandez kuwa mbioni kuisha mwishoni mwa mwezi huu, hata hivyo Barcelona wamesema kwamba hawatashawishika tena kumuongezea mkataba kutokana na mkurugenzi huyo kutofanikisha matarajio ya klabu hasa upande wa usajili.
Mkurugenzi huyo wa michezo anayemaliza muda wake akabiliwa na upinzani juu ya kuondoka kwa Neymar mwaka jana katika uhamisho wa rekodi ya duniani akielekea Paris Saint-Germain.
-
Jonny Evans ajiunga na Leicester City
-
Liverpool walazimisha usajili wa Nabil Fekir
-
Juventus wamchukua jumla Douglas Costa