Serikali imeanza majadiliano na Wawakilishi kutoka Barrick Gold Corporation juu ya biashara ya madini yanayochimbwa katika migodi na kampuni hiyo hapa nchini ili kuweza kufikia muafaka na taratibu zilizokiukwa.

Kamati hiyo maalumu iliyoundwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli kwaajili ya majadiliano inaongozwa na Waziri wa Sheria na Katiba, Prof. Palamagamba Kabudi wakati Kamati ya Barrick Gold Corporation  ikiongozwa na Afisa Mwendeshaji Mkuu, Richard Williams.

Aidha, akizungumza kabla ya kuanza kwa majadiliano hayo Prof. Kabudi amesema Kamati yake imejipanga vizuri kujadiliana na Barrick Gold Corporation juu ya madai ya Tanzania  katika biashara hiyo ya madini na itahakikisha inasimamia maslahi ya Tanzania ipasavyo.

Kwa upande wake, Richard Williams ameshukuru kuwepo kwa majadiliano hayo huku akisema Kampuni ya Barrick Gold Corporation imeyapokea madai ya Tanzania  kwa mtazamo chanya na ipo tayari kujadiliana na kufikia makubaliano yenye maslahi kwa pande zote mbili.

 

 

Manula kuchezea rasmi klabu ya Simba
Soma povu la Diva kuhusu utimu Kiba