Rais wa Gambia, Adama Barrow amemteua Fatoumata Jallow-Tambajang kuwa Makamu wa Rais wa nchi hiyo. Huo ni uteuzi wa kwanza tangu Barrow alipochukua madaraka Januari 19

Barrow bado yuko nchi jirani ya Senegal alikotafuta hifadhi kwa sababu za kiusalama, amesema amemteua mwanamke huyo Fatoumata Jallow-Tambajang kushika wadhifa huo, kwa sababu ya kushughulikia usawa wa kijinsia.

Fatoumata alikuwa mfanyakazi wa zamani wa Shirika la Mpango wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa, UNDP, ni mtu muhimu ambaye aliviunganisha vyama vya upinzani kusimama pamoja katika uchaguzi dhidi ya kiongozi wa zamani wa Gambia, Yahya Jammeh.

Mwishoni mwa mwaka uliopita, Fatoumata fanya mahojiano na gazeti la The Guardian na kusema kuwa  atamfungulia mashtaka ya uhalifu Jammeh. Muda mfupi baada ya tangazo hilo, Jammeh ambaye sasa yuko uhamishoni Equatorial Guinea, alibadili uamuzi wake wa awali wa kukubali kushindwa katika uchaguzi wa Disemba Mosi, na kudai kulikuwepo na udanganyifu, hali iliyochochea mzozo wa kisiasa.

Aidha, Fatoumata ameitaka tume ya taifa ya kudhibiti mali, kuzirejesha mali na ardhi ambayo inadaiwa kuchukuliwa na Jammeh kwa maslahi yake mwenyewe

Video: CUF sasa yamlilia mkuu wa majeshi, Vijiji 8,000 nchini kupatiwa umeme
Granit Xhaka Ahojiwa Na Polisi