Kiungo wa klabu ya West Bromwich Albion, Gareth Barry amevunja rekodi ya mchezaji aliyecheza michezo mingi ya ligi kuu ya Uingereza iliyokuwa ikishikiliwa na winga mshambuliaji wa zamani wa Manchester United Ryan Giggs.

Garreth Barry aliyeanza kucheza soka la kulipwa mwaka 1998 amevunja rekodi hiyo kwa kucheza mchezo wake wa kulipwa wa 633 uliopigwa jana usiku katika uwanja wa Emirates dhidi ya klabu ya Arsenal ambapo Asenal ilishinda mabao 2-0.

Barry hadi sasa amecheza ligi kuu ya Uingereza kwa miaka 19 na sasa anakuwa amempita Ryan Giggs ambaye alikuwa akishikilia rekodi ya kucheza michezo 632 ya ligi hiyo.

Mara baada ya mchezo kati ya Arsenal na West Bromwich kocha wa Arsenal, Arsene Wenger alitoa zawadi ya jezi ya Arsenal kwa Barry yenye namba 633 mgongoni ambayo ni idadi ya mechi alizocheza mchezaji huyo katika ligi ya Uingereza akiwa na timu tofauti.

Barry mwenye umri wa miaka 36 amepewa jezi hiyo ikiwa imesainiwa na wachezaji wa Arsenal ikiwa ni sehemu ya kumbukumbu kwake.

 

DC na RC waonywa utumiaji mbovu wa madaraka
Ben Pol ataja chanzo cha kumzimia simu Ebitoke