BASATA imelifungulia Shindano la Miss Utalii Tanzania baada ya waandaaji kutekeleza kwa vitendo maagizo na maelekezo yote yaliyotolewa na Baraza hilo.
Basata iliwataka kuimarisha mfumo wa ungozi na mfumo wa mashindano kitu ambacho tayari bodi ya mashindano imefanya mabadiliko hayo kwa kuanzisha organisation structure ambapo sasa kuna Governing Board na Executive Board na Management Team.
Aidha, kukiwa na mgawanyo wa madaraka kuanzia chini hadi juu, pia wameanzisha mfumo mpya wa mashindano hayo, ambapo sasa lina kuwa ni shindano la kimataifa la Miss Utalii Tanzania yani Miss Tourism Tanzania International Ageant, ambalo washiriki kutoka duniani kote watawakilisha nchi zao kuwania taji la kimataifa la Miss Tanzania International.
Hata hivyo, washirikï kutoka mikoa yote ya tanzania watawakilisha mikoa yao katika fainali za kanda, na hatimaye washindi wakiwakilisha kanda zao katika fainali za kimataifa wakiwanîa taji la Miss Utalii Tanzania yaani Miss Tourism Tanzania.