Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA), limemuandikia barua Shilole ikielezea uamuzi wa baraza hilo kumfungia kushiriki masuala ya Muziki kwa muda wa mwaka mmoja kwa kosa la kukiuka maadili ya Tanzania wakati akifanya onesho lake nchini Ubelgiji miezi kadhaa iliyopita.

Akiongea na E- Fm radio ya Dar es Salaam, Afisa wa BASATA alieleza sababu zilizopelekea baraza hilo kumuadhibu Shilole ikiwa ni adhabu inayomfungia ndani na nje ya nchi.

“Adhabu imetolewa kwa ajili ya kuweza kujirekebisha tabia hiyo ambayo inakiuka maadili ya kazi ya sanaa lakini na maadili ya nchi vilevile. Kwa sababu kama unakumbuka Bunge la Bajeti mwaka huu , naibu waziri alikuwa ameliomba radhi bunge na watanzania kutokana na kile kilichotokea katika onesho la Shilole,” alisema afisa huyo wa BASATA.

“Katika ile statement ya naibu waziri alisema kwamba taratibu zote za kanuni na sheria zitafuatwa kuweza kuangalia suala la Shilole linakuwaje. Kwa hiyo kwa mujibu wa sheria, kanuni na ukiangalia katiba ya nchi ambayo inazungumzia suala zima la maadili, kwa maana ndiyo imefikiwa hivyo kwamba aweze kujifunza,” Aliongeza.

Awali, Shilole alijitetea akidai kuwa upya wa vazi alilofanyia onesho ndilo lililomponza huku akirusha lawama kwa aliyesambaza picha hizo kwenye mitandao kutoka ughaibuni.

“Kiukweli kwa sababu hili jambo limetokea inatakiwa nguo ninapoinunua niwe naifanyia training kwanza kabla ya kwenda jukwaani, kwahiyo kwa sababu ile nguo ilikuwa mpya kwangu na sikuweza kuijua vizuri yaani hii nguo nimeikuta huku huku, nguo imekuja kunitokea bahati mbaya wakati niko kwenye performance, ilitatuka wakati niko kwenye motion,” Shilole aliiambia Clouds FM.

Xavi Amuomba Jambo Muhimu Guardiola
Lowassa: Tutashinda Bila Kashfa Na Matusi