Syria imerejesha kwa Ufaransa tuzo ya Légion d’honneur aliyopewa rais Bashar al-Assad, ikisema kuwa haiwezi kuchukua tuzo hiyo kwa taifa ambalo limekuwa ni mtumwa wa Marekani.
Syria imefikia hatua hiyo siku moja mara baada ya Ufaransa kusema kuwa adhabu ya kuikataa tuzo hiyo inakaribia ambayo inaheshima kubwa.
Aidha, hivi karibuni Ufaransa ilijiunga na Uingreza,na Marekani katika kuishambulia Syria kufuatia madai ya kutumia silaha zenye sumu dhidi ya raia wake.
“Wizara ya mambo ya nje imerudisha kwa Jamhuri ya Ufaransa tuzo ya Légion d’honneuri aliyopewa rais Assad, Sio heshima kwa rais Assad kuvaa tuzo iliyotolewa na taifa la utumwa na mshiriki wa taifa la Marekani linalounga mkono ugaidi,”imesema Wizara hiyo
Hata hivyo, Takriban watu 3,000 kila mwaka hutuzwa tuzo hiyo ya hadhi ya juu kwa huduma walizotoa kwa Ufaransa ama kwa kutetea haki za kibinadamu, uhuru wa kujieleza ama sababu kama hizo.