Maoni ya aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa katika serikali ya awamu ya nne, Bernard Membe kuhusu utendaji wa serikali ya Rais John Magufuli yanaendelea kuzua gumzo, na sasa yamemuamsha Mbunge wa Nzega Mjini, Hussein Bashe.

Bashe amemkosoa Membe kwa kauli zake akidai kuwa hoja alizozitoa ni za mwanasiasa Mufilisi, huku akidai kuwa asubiri awamu nyingine agombee urais ili aunde serikali yake aliyoifananisha na ya Vasco Dagama.

Mbunge huyo ameenda mbali na kumtuhumu Membe kwa kutumia fedha za umma wakati akiwa madarakani ofisi yake ilitumia fedha za umma kusafiri kwenda nchi za nje na wapenzi wao.

Hivi ndivyo alivyoandika Bashe kwenye ukurasa wake wa Facebook: 

Membe Amuache Ndg Magufuli Afanye kazi.

Membe amekua waziri for ten yrs ametimiza wajibu wake amuache Ndg Magufuli atimize wajibu wake. Aliomba Urais Hajateuliwa asubiri 2020 or 2025 ili akipita aanzishe uvasko dagama tena.

Hoja kuwa serekali haijapungua ama kubwa or ndogo ama hoja kuwa Safari za nje nimuhimu na Rais amekosea kufuta ama kupunguza ni hoja ya mwanasiasa muflisi .

Membe amekua sehem ya mfumo dhaifu ulotufikisha hapa kama Taifa,Amefaidika na safari za nje yy binafsi bila manufaa kwa nchi,Membe akumbuke kila Rais ana Vission yake Magufuli believes matatizo ya Taifa letu yatamalizwa na sisi wenyewe kwa kudhibiti matumizi ya Hovyo na yasiyoyalazima na si kwa safari za Ulaya na kuendeleza Tabia ya Kuwa Omba omba.

Ni muhimu membe afahamu magufuli ana style yake tutampima kwx matokeo as of now hatujaona athari za safari labda membe kama yy binafsi anatakiwa aseme kufutwa safari kuli muathiri yy binafsi kwakukosa nafasi ya Ukatibu mkuu wa Common wealth thats why leo anakosoa.

Tunafaham maamuzi mengi ya magufuli kwa sasa hayatafurahisha wengi walofaidika na Miradi kama NIDA Pesa za Gadafi, walofaidika na Matumizi Mabaya ya Madaraka ktk Awamu ya nne,Majipu mengi yanayosubiri Kutumbuliwa ama yaliyotumbuliwa yatafanya jitihada kukosoa muelekeo wa Serekali ya awamu ya Tano.

Hoja ya kutokua na mabalozi magufuli hana siku 100 yy amekua waziri wa mambo ya nje for 8 yrs hakuona umuhimu wakati huo? Kuwx na balozi kwenye nchi ni jambo Mtambuka na hasa linatazamwa zaidi kiuchumi na kisiasa .

amekua mmoja wa mawaziri walouwa foreign relation yetu wakati wake kumekua na malalamiko mengi juu yx mis use of funds ktk wizara yake,kipindi chake safari za nje walisafirishwa ma girlfirend kwa kutumia Pesa za Umma.

Nimuhimu membe aheshimu Vission ya Magufuli na style yake inafahamika ameathiriki directly or Indirect na mchakato wa Majipu na kufunga safari za nje.

Binafsi kama mbunge naunga mkono style ya magufuli ya uongozi aliwahi kusema Sankara ” You cannot carry fundamental change without a certain amount of Madness”

Mabadiliko anayofanya sasa Ndg Magufuli yanahitaji Roho Ngumu,wendawazimu kidogo, Kuungwa mkono na wananchi wx kawaida kwani walofaidika na udhaifu wa awali watajitahidi kutaka kuzuia mabadiliko yoyote ambayo yanamfaidisha aliekuwa akinyonywa hapo awali tutasikia watu wa aina ya membe wengi kwakua style ya magufuli inaathiri mfumo wao wakuwanyonya wengi na wachache kufaidika.

Wassalaam.

Kanye West amalizana na hili, adai amefunika wote
Idris na wema wanatarajia mtoto, idris amuandika ujumbe mtamu akimuita 'wife'