Mbunge wa jimbo la Nzega Mjini, Hussein Bashe ameitahadharisha kuhusu sera ya elimu bure inaotolewa na Serikali ya Awamu ya Tano kutojikita katika idadi ya wanafunzi bali ubora wa elimu husika.
Akiongea jana na waandishi wa habari, Bashe alieleza kuwa serikali za awamu zote zilizopita zilijikita zaidi katika kuongeza idadi ya wanafunzi huku ubora wa elimu ukiachwa nyuma.
Mbunge huyo aliishauri serikali inayoongozwa na Rais John Magufuli kurudi mezani na kujipanga upya ili kuboresha mfumo wa elimu kwani tayari makosa yameshafanyika katika utekelezaji wa ‘elimu bure’.
Kadhalika, Bashe alipinga mtazamo wa utoaji elimu bure akidai kuwa elimu hiyo haitolewi bure bali inagharamiwa kwa kodi wanazolipa wananchi.
“Kama nchi tuko kwenye wakati mgumu. Si dhambi tukikiri tulifanya kosa katika kutekeleza mfumo wa elimu bure na hatujui tunataka kujenga taifa la namna gani kwa sababu tulishafanya makosa awali. Tunapaswa kukaa mezani na kuanza upya,” alisema.
kuhakikisha kuwa sera ya elimu bure isiishie kuongeza idadi ya wanafunzi wanaodahiliwa, bali iangalie ubora na ufaulu wa wanafunzi.
Hata hivyo, majibu ya utafiti wa Taasisi ya Twaweza yaliyotolewa jana yameonesha kuwa wananchi wengi wanaamini kuwa elimu Bure itasaidia kuboresha mazingira ya ufundishaji na elimu kwa ujumla.
“Asilimia 76 ya wananchi wanaamini kuwa utolewaji wa elimu bure utaongeza ubora wa elimu kwa kuboresha mazingira ya kufundishia (asilimia 55),” utafiti huo umeeleza.
Utafifi huo umeonesha kuwa asilimia 15 ya wananchi waliofikiwa walisema elimu bure haitaboresha elimu, kwa kuwa kuongezeka kwa uandikishwaji wa wanafunzi kutatumia rasilimali/fedha.