Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Bashiru Ally amewataka wanachama wa chama hicho kumuunga mkono Mbunge wa Bukoba Mjini (CHADEMA), Wilfred Lwakatare, ili wweze kumng’oa katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020.
Akizungumza na baadhi ya wanachama na viongozi nje ya ofisi za CCM Mkoa wa Kagera, mjini Bukoba, leo Desemba 22, 2018 Dkt. Bashiru ametaja sababu za kuunga mkono kuwa Wilfred Lwakatare ni Mbunge halali, muungwana na hapotoshi wananchi.
Hata hivyo, pamoja na sifa hizo amesema mbunge huyo ajiandae kung’oka mwaka 2020, huku akiagiza kabla ya kuondoka mkoani Kagera apatiwe maelezo ya sababu ya kufa kwa kilimo cha zao la chai alilodai lilikuwa mkombozi kwa wananchi ambao walifanikiwa kujiongezea kipato na kusomesha watoto
Dkt. Bashiru amesisitiza kuwa Taifa lina uwezo wa kujitegemea huku akitaja baadhi ya changamoto zilizopo zikiwemo ukosefu wa ajira na kuagiza wakuu wa mikoa nchini kutatua kero za wananchi pamoja na kuondoa uonevu kwa wafanyabiashara wadogo.
-
Ndege ya kisasa mpya ATCL kutua nchini, JPM kuipokea
-
Waziri Hasunga asimikwa kuwa Chief Nzunda, asema hakuna mbadala wa CCM
-
Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Desemba 23, 2018
Katibu mkuu huyo amesema amekwenda mkoani Kagera, ambako ni nyumbani kwake kwa ajili ya mapumziko ya mwishoni mwa mwaka yatakayokwenda sambamba na ziara hadi Januari 2, 2019 kwa kutembelea wilaya mbalimbali za mkoa huo