Waziri wa Viwanda na Biashara, Innocent Bashungwa ametangaza ukomo wa bei ya barakoa nchini Tanzania kuwa ni 1,500 ambayo wengi wataweza kumudu.
Bashungwa amesema serikali itachukua hatua kwa Taasisi zisizo za kiserikali (NGOs) zinazouza barakoa kwa gharama kubwa.
Bashungwa alitoa taadhari hiyo mkoani Arusha alipotembelea Viwanda vya kuzalisha nguo vya Sunflug na A to Z kuangalia hali ya uzalishaji wa barakoa katika Viwanda hivyo.
Aliongeza kusisitiza barakoa zote ziuzwe kwa bei isiyozidi 1,500 badala ya bei ya sasa ilikuwa sokoni ya 2,500 ambayo watanzania wengi inawapa changamoto ya kumudu.