Basi la kampuni ya Kilimanjaro linalofanya safari kutoka Tunduma kwenda Dar es Salaam limepata ajali maeneo ya Senjele mkoani Songwe.

Basi hilo limepata ajali leo Jumatatu Machi 14, 2022 asubuhi wakati likielekea Dar es Salaam.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe, Rashid Ausi amethibitisha kutokea ajali hiyo akisema anaelekea kwenye eneo la tukio.

Bado hakuna taarifa za vifo wala majeruhi zilizoripotiwa mpaka sasa.

Endelea kufuatilia Dar24 kupata taarifa zaidi.

Young Africans: Tutamuuza yeyote utaratibu ukifuatwa
RS Berkane wamshtaki Ndala CAF