Polisi waliokuwa katika Doria maeneo ya barabara kuu ya Nairobi – Mombasa jana wamekamata basi la kanisa la PEFA likiwa na Misokoto 230 ya bangi iliyokuwa imewekwa kwenye eneo la mizigo.

Imeelezwa kuwa basi hilo lilikuwa limesafirisha waombolezaji kutoka kilifi kwenda Homa Bay na wakati wa kurudi ndipo bangi hiyo ikapakizwa.

Tayari dereva wa basi hilo pamoja na watu wengine wawili wametiwa mbaroni ili kusaidia polisi kwenye uchunguzi wa kisa hicho.

Hata hivyo bangi hiyo inakadiriwa kuwa na thamani ya zaidi ya shilingi milioni moja.

Serikali yashinda rufaa, ma DED kusimamia uchaguzi
Magufuli amuwashia moto Mbarawa