Bayern Munich inataka kuwasilisha ofa mpya ya Pauni 94.6 Milioni kwenda Totenham ili kumsajili Mhambuliaji wa wababe wa jijini London Harry Kane katika dirisha hili.

Awali, ilielezwa kwamba Kane huenda akaendelea kusalia Spurs kwa sababu mwenyekiti wa timu hiyo Daniel levy hataki kutoa majibu juu ya ofa zilizowasilishwa na mabosi wa Munich.

Munich awali iliwasilisha ofa ya mwishoni mwa juma lililopita na kuitaka Spurs kutoa majbu hadi kufikia ijumaa lakini hakukuwa na majibu yoyote na levy akapanda zake ndege kwenda nchini Marekani huku nyuma akiacha watu njia panda.

Mbali ya yote hayo Bayern inaonekana kuwa haijakata tamaa na ìmeamua kuwasilisha ofa hiyo mpya, huku ripoti zikieleza kwamba wameshamtafutia hadi mjengo wa kukaa ambao upo nje kidogo ya Jiji la Munich.

Kane ambaye mkataba wake wa sasa unamalizika mwakani, anawindwa na mabingwa hao watetezi wa Bundesliga kutokana na uwezo wake mkubwa wa kutupia wavuni.

Kane amefunga mabao 280 katika mechi 435 alizoitumikia Tottenham tangu msimu wa 2011-12 na msimu uliopita alifungia mabao 32′ katika mechi 49 za michuano yote.

Mshambuliasji huyo pia ndiye kinara wa muda wote wa timu ya taifa ya England akiifungia mabao 56 katika mechi 83.

128 wawekewa Puto Tumboni, watatu wakubali yaishe
Polisi kuendeleza ushirikishaji jamii kutokomeza uhalifu