Mabingwa wa soka nchini Ujerumani FC Bayern Munich, wamekamilisha usajili wa kiungo mshambuliaji kutoka nchini Chile, Arturo Vidal kwa kukubaliana na mabingwa wa soka nchini Italia Juventus.

Mtendaji mkuu wa FC Bayern Munich Karl-Heinz Rummenigge amethibitisha taarifa hizo muda mchache uliopita alipokutana na waandishi wa habari kabla ya safari ya kikosi cha The Bavarians kuelekea nchini China kwa matayarisho ya msimu mpya wa ligi.

Rummenigge amesema makubaliano ya kusajili kwa Arturo Vidal yametuama kati ada ya uhamisho wa paund million 24.5.

Amesema Vidal huenda akajiunga na wachezaji wenzake juma lijalo baada ya kukamilisha utaratibu wa kufanyiwa vipimo vya afya.

Amesema tayari wameshakubaliana maslahi binafsi na Vidal na atakua akipokea mshahara wa paund 90,000 kwa juma.

Vidal aliuonmba uongozi wa Juventus ruhusa na kuondoka na kwenda kusaka maisha mahala pengine duniani, na ndipo FC Bayern Munich walipopata nafasi ya kupenyeza sera za kutaka kumsajili.

Kundoka kwa Vidal kunaifanya Juventus kuwapoteza wachezaji watatu mpaka sasa ambao waliisaidia klabu hiyo kufanya vyema katika ligi ya nchini Italia pamoja na barani Ulaya.

Tayari mshambuliaji Carlos Tevez ameshaondoka na kurejea nyumbani kwao Argentina kujiunga na klabu ya Boca junior sambamba na Andrea Pirlo aliyemaliza mkataba wake ambapo ameelekea nchini Marekani kujiunga na New York city FC.

Ronaldo Amuwakia Kocha Wake Benitez
Profesa Tibaijuka Azomewa Tena, Wananchi Wamkejeli Na Viroba