Mkurugenzi Mtendaji wa Klabu Bingwa nchini Ujerumani FC Bayern Munich, Oliver Kahn amethibitisha kwamba, hawatakuwa kwenye kinyang’anyiro cha kuiwania saini ya Mshambuliaji kutoka Norway Erling Haaland.

Bayern wanakabiliwa na sintofahamu kuhusu mustakabali wa mshambuliaji Mshambuliaji waa Robert Lewandowski, lakini Kahn hatarajii mchezaji huyo wa kimataifa wa Poland kuondoka hivi karibuni.

Kahn akizungumza na Suddeutsche Zeitung amesema, “Tunaye Robert Lewandowski. Atafunga mabao 30 au 40 zaidi kwa miaka kadhaa ijayo, hivyo hatumhitaji Erling Braut Haaland.”

Klopp: Tulistahili kufungwa

Kutokana na hali hiyo, Manchester United, Barcelona, ​​Paris Saint-Germain, Real Madrid na Manchester City wanapunguziwa ushindani kumpata Haaland, huku timu hizo zikisemekana zinataka kumsajili mchezaji huyo wa kimataifa wa Norway mwaka ujao.

Haaland amefikisha mabao 76 katika michezo 75 pekee ya Dortmund kwenye mashindano yote, ikijumuisha mabao 19 kutoka mechi 16 za msimu wa 2021-22.

Shearer: Wamekubaliana kumtosa Aubameyang
Klopp: Tulistahili kufungwa