Uongozi wa Klabu Bingwa nchini Ujerumani FC Bayern Munich utapiga hatua zaidi katika mbio za kutaka kumsajili Mshambuliaji kutoka England na Klabu ya Tottenham na England, Harry Kane, huku ukiwatuma watendaji wake wawili kwenda London.
Mtendaji Mkuu, Jan-Christian Dreesen na Mkurugenzi wa Ufundi, Marco Neppe wanajiandaa kufanya mazungumzo na mwenyekiti wa Tottenham, Daniel Levy ambaye amerudi kutoka katika ziara timu hiyo nchini ya Australia na Kusini Mashariki mwa Asia.
FC Bayern Munich wameendelea kujiamini kuhusu kukamilisha mpango huo wa kumnasa Kane, ambaye yuko katika mwaka wake wa mwisho wa mkataba na Spurs.
Waliongeza ofa yao ya mwisho ambayo ilikuwa ikikaribia Pauni Milioni 70 (sawa na Sh milioni 220), lakini wanahisi kuwa Spurs huenda sasa wakakubali baada ya mabosi hao kwenda London kwa mazungumzo zaidi.
Aidha, kwa mara ya kwanza Rais wa Bayern Munich, Herbert Hainer ameibuka hadharani na kukiri kuwa klabu yake inataka kumsajili Harry Kane na kumuelezea mshambuliaji huyo wa Tottenham kuwa ni mchezaji anayevutia.
Kane amebakisha mwaka mmoja katika mkataba wake na Tottenham na yuko mbioni kwenda kwa mabingwa wa Bundesliga katika kipindi hiki cha majira ya joto.