Serikali ya Burundi imevifungia vyombo vya habari vya Voice of America (VOA) na British Broadcasting Corporation (BBC) kurusha matangazo yao nchini humo kwa muda wa miezi sita kuanzia Mei 7 mwaka huu.
Uamuzi huo ni kufuatia na vyombo hivyo kutofuata sheria zinazotoa muongozo wa uandishi habari nchini humo na kukiuka maadili ya kikazi.
Inaishutumu BBC kwa kushindwa kumwajibisha mwanaharakati wa Burundi katika mahojiano aliyofanyiwa katika idhaa ya kifaransa ya shirika hilo.
Taarifa hiyo imetolewa na Mtandao wa habari nchini humo.
Aidha Mamlaka ya kudhibiti Mawasiliano nchini humo wamesema BBC imefungiwa kwa kufanya mahojiano na mwanaharakati wa Burundi katika moja ya vipindi vyao ambapo mahojiano hayo yamechukuliwa kama ni ya kichochezi dhidi ya Rais wa nchi hiyo, Piere NKurunziza.
VOA nayo imesitishwa kurusha matangazo yake mara baada ya kutumia tovuti ya mtandaoni iliyofungiwa tangu mwaka 2015 kurusha matangazo yake nchini humo.
Hata hivyo Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano nchini humo imesema inakaribisha malalamiko yeyote kutuka kwa vyombo hivyo vilivyofungiwa kurusha matangazo yake nchini humo.
Nchi hiyo inajitayarisha kwa kura ya maoni Mei 17 ambayo huenda ikamuongezea muda wa kuhudumu rais Pierre Nkurunziza hadi mwaka 2034.