David Beckham amewajibu wanaosema Inter Miami inapanga matokeo katika Ligi Kuu ya Marekani ni kama pongezi kwao walioamua kuitoa katika njia tofauti baada ya kubeba taji kwa mara ya kwanza katika historia ya klabu hiyo.
Shutuma hizo za watu zilikuja baada ya nyota wa zamani wa Barcelona, Lionel Messi, Sergio Busquets na Jordi Alba kuisaidia kushinda mechi nane mfululizo.
Inter Miami iliifunga FC Cincinnati kwa mikwaju ya penalti 5-4 katika fainali nyingine ya US Open Cup baada ya kusavwazisha mabao mawili na mechi kumalizika kwa mabao 2-2 kabla ya mechi hiyo kuongezewa dakika 30.
Timu hiyo ilibeba taji la kwanza baada ya kuifunga Nashville kwa mkwaju wa penalti na Beckham alijibu kufuatia kauli za wapinzani.
Beckhamn alisema kwamba: “Kila mnara Messi anapofunga bao, Sergio Busquets anapotoa pasi nzuri, Jordi Alba anavyokimbia kwa kasi eti tunapanga matokeo?
Nadhani hizo ni pongezi wametoa kwetu. Unapowaangalia wachezaji hawa wanavyocheza soka ni burudani tosha. Kila kitu. Kuhusu wao wanapokuwa uwanjani kinavutia kuangalia.”
Inter Miami itacheza fainali nyingine ya US Open Cup dhidi ya Houston Dynamo, Septemba 27, mwaka.
Mpaka sasa timu hiyo imecheza mechi nane bila ya kufungwa tangu Messi, Busquets ana Alba waliposajiliwa katika dirisha hili la usajili.