Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Petroli – EPRA, nchini Kenya itatangaza bei mpya za mafuta zinazotokana na Kodi mpya ya Ongezeko la Thamani kwenye bidhaa za petroli, ambayo itakuwa asilimia 16, kufuatia kupitishwa kwa Sheria ya Fedha, 2023.
Kwa mujibu wa Citizen Digital, itakumbukwa juni 26, 2023 Rais Dkt. William Ruto alitia saini sheria muswada wa Fedha wa 2023 wa kuwasilisha VAT ya asilimia 16 kwa bidhaa za petroli.
Kwa hivyo, kupelekea EPRA leo tarehe 30 Juni 2023 itatoa bei mpya iliyopitiwa ya mafuta ya petroli kulingana na muswada wa fedha wa 2023.
Hapo awali, bidhaa za Petroli zilitozwa asilimia 8 ya VAT huku hayo yakijiri takriban wiki mbili baada ya EPRA kutangaza bei mpya za mafuta kwa mwezi wa Juni-Julai ambapo mabadiliko ya bei yangeanza Juni 15 hadi Julai 14, 2023.
Juni 14, Mamlaka ilitangaza kuwa bei ya petroli ilipungua kwa Sh0.66 hadi rejareja kwa Sh182.04, huku dizeli ikipunguzwa kwa Sh1.12 hadi 167.28 jijini Nairobi na kupelekea bei ya mafuta ya taa kuongezwa kwa Sh0.35 hadi rejareja kwa Sh161.48.
Hata hivyo, wakati kiwango kipya cha VAT kikianza kutekelezwa, bei ya petroli huenda ikauzwa kwa Sh196.60 jijini Nairobi, dizeli Sh180.66, na Mafuta ya taa kwa Sh174.39.