Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji – EWURA, imetangaza bei kikomo za bidhaa za mafuta ya petroli hapa nchini zitakazotumika kuanzia hii leo Jumatano Septemba 6, 2023 ambapo bei za rejareja za mafuta katika Mkoa wa Dar es Salaam ni Shilingi 3,213 kwa Petroli, 3,259 Dizeli na 2,943 kwa mafuta ya Taa.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkugenzi wa EWURA, Dkt. James Mwainyekule imeeleza mabadiliko hayo yanatokana na kupanda kwa gharama za mafuta katika soko la dunia kwa hadi asilimia 21, gharama za uagizaji wa mafuta hadi asilimia 62 na maamuzi ya kisiasa katika nchi zinazozalisha mafuta kwa wingi (OPEC+).

Aidha, taarifa hiyo imefafanua kuwa Wafanyabiashara wa bidhaa za mafuta kwa rejareja wanatakiwa kuuza mafuta kwa bei zilizoainishwa na kwamba hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya yoyote atakayekiuka agizo hilo na kwamba wazingatie bei kikomo kwa eneo husika ambazo zinapatikana kupitia simu za mkononi kwa kupiga namba 15200#.

Kwa mujibu wa Sheria ya Mafuta ya mwaka 2015, kifungu namba 166, bei za bidhaa za mafuta ya petroli zitaendelea kupangwa na soko. EWURA itaendelea kuhamasisha ushindani kwa kutoa taarifa za bei kikomo za bidhaa za mafuta na Kampuni za mafuta ziko huru kuuza bidhaa za mafuta ya petroli kwa bei ya ushindani isipokuwa bei hizo zisizidi bei kikomo.

Bei zote kwa kila eneo zimeorodheshwa kupitia Jedwali hapo chini.

Bosi Simba SC aitumia salamu Al Ahly
Tabora United yachimba mkwara Ligi Kuu