Wakati ujenzi wa daraja Kiyegeya barabara ya Morogoro,Dodoma ukiendelea baada ya kuzolewa na maji baadhi ya abiria na madereva waliokwama kuendelea na safari wamesema wanauziwa chakula kwa bei ya juu kuliko awali

Kwamujibu wa Gazeti la mwananchi, wakizungumza na wananchi kwa nyakati tofauti wamesema kuwa kwa sasa sahani moja ya chakula inauzwa 3500 hadi 4500 badala ya shilingi 2000 na vinywaji vinauzwa 1000 hadi 1500 kutoka 500 hadi 700.

Naye Mohamed Iddi anayeelekea wilayani Mpwapwa amesema alipanda basi jana huku abiria wakiaadiwa wakifika eneo hilo watahamishiwa katika usafiri mwingine ahadi ambayo imeota mbawa, ambapo Jonas Mdabi amesema kuwa shida katika eneo hilo ni huduma ya choo na eneo la kuoga.

Daraja hilo lililopo Gairo linalounganisha mikoa ya Dodoma na Morogoro lililosombwa na maji juzi Jumatatu saa 9 alasiri kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha.

Vijana 7 wafanyabiashara wafariki dunia kwa ajali mbaya
Biden afungua jumanne maalumu ya ushindi