Beki wa zamani wa klabu ya Stoke City, Dionatan Teixeira amefariki dunia akiwa na miaka 25 kutokana na kile kinachoaminika kuwa mshtuko wa moyo.

Dionatan Teixeira alijiunga na Stoke 2014 baada ya kufanyiwa majaribio klabu kadha za Ligi ya Premia ikiwemo Manchester City lakini mchezaji huyo wa Brazil hakufanikiwa katika ligi ya Uingereza kutoka na kusumbuliwa na majeraha. Aliichezea Stoke mechi mbili pekee katika miaka mitatu aliyokaa katika klabu hiyo.

Kwa mujibu wa klabu ya FC Sheriff ya Moldovia ambayo alikuwa anaichezea inayoshiriki Europa League Teixeira alikuwa Brazil alipougua na kufariki Jumapili.

Klabu ya FC Sheriff ilishinda kombe la ligi nchini humo imesema Dionatan Teixeira atabaki katika mioyo yao daima

 

Mwalimu Mkuu amcharaza viboko mwalimu mwenzie
Kigwangalla atumbua jipu kwa kufuatiliwa na watu wasiojulikana