Nchini Belarus wafuasi wa upinzani wamefanya maandamano katika mji mkuu wa nchi hiyo, Minsk wakitaka Rais Alexander Lukashenko kuachia madaraka.

Hivi karibuni nchi hiyo ilifanya uchaguzi mkuu ambapo kwa mujibu wa matokeao rasmi Rais Lukashenko alitangazwa kuwa mshindi.

Mara baada ya kutangazwa kwa matokeo hayo maelfu walikusanyika wakitaka Rais Lukashenko kuondoka madarakani licha ya uwepo wa Polisi katika eneo hilo.

Ikumbukwe Rais Lukashenko aliongoza Belarus kwa miaka 26 na alishinda uchaguzi kwa zaidi ya 80% na mgombea wa upinzani, Svetlana Tikhanovskaya alipata 10% ya kura zilizopigwa

Kanda athibitisha kuondoka Simba SC
Video: FC Bayern Munich bingwa UEFA