Kiungo Mshambuliaji Jude Bellingham na Lewis Dunk wameondolewa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya England kinachojiandaa na mchezo wa kuwani kufuzu Fainali za Mataifa ya Ulaya ‘Euro 2024’ dhidi ya Malta na Macedonia Kaskazini.
Bellingham aliyesajiliwa na Real Madrid bado anauguza jeraha la msuli wa paja ambalo lilimweka nje kwenye mechi ya mwisho ya Borussia Dortmund, waliposhindwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Ujerumani, Bundesliga, baada ya sare ya 2-2 nyumbani na Mainz.
Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 19 ataripoti St George’s Park ili kupata matibabu zaidi, lakini hatacheza mechi yoyote, taarifa ya timu ilithibitisha.
Beki wa Brighton, Dunk amejiondoa kwenye kikosi kutokana na jeraha na hatasafiri katika kituo cha taifa cha soka mchezaji pekee kutoka kikosi cha awali cha wachezaji 25 cha kocha Gareth Southgate ambaye kwa sasa hatastahili kujiunga.
Wachezaji wa England walianza kukusanyika pale St George’s Park Jumapili, wakijiandaa kwa safari ya Ijumaa kucheza na Malta huko Ta’Qali na mechi ya Jumatatu dhidi ya Macedonia Kaskazini kwenye uwanja wa Old Trafford.
Declan Rice wa West Ham, ambaye alinyakua taji la Ligi ya Europa Conference katikati ya wiki, atajiunga siku zijazo, kama vile wachezaji watano wa kikosi cha Manchester City walioshinda Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Jack Grealish, John Stones, Phil Foden, Kyle Walker na Kalvin Phillips wote jana Jumatatu walikuwa sehemu ya gwaride la mabasi ya City mjini Manchester kabla ya kuripoti kambini.
Katika video iliyotumwa kwenye akaunti za mitandao ya kijamii ya timu ya taifa ya England Jumapili (Juni 11), Southgate alisema: “Tuna mazoezi machache kidogo na tunasubiri wachezaji wote kuja.
“Wote wanajiweka katika hali nzuri lakini hatufanyi mazoezi na timu katika kipindi hicho na lazima urekebishe mwili wako.
“Nadhani tulichoonyesha katika miezi michache iliyopita ni kwamba sisi ni timu ambayo sasa inaweza kuwa timu bora zaidi duniani.
“Tulionyesha hilo kwenye Kombe la Dunia na kwa hakika tulionesha hilo kwa kushinda kwa Naples (ushindi wa 2-1 dhidi ya Italia Machi), ambao ulikuwa mchezo muhimu kwetu sio tu katika suala la kufuzu lakini kwa kujiamini na kuweka alama fulani kwa kile tulichonacho kama timu.