Beki wa Klabu ya Chelsea, Ben Chilwell amesaini mkataba wa miaka miwili kuendelea kukipiga kwenye timu hiyo akiahidi kujituma zaidi.

Beki huyo amecheza mechi 81 katika mashindano yote tangu alipotua 2020 na sasa atakipiga Stamford Bridge hadi 2027.

Chilwell atakuwa akilipwa mshahara wa Pauni 200,000 kwa juma baada ya kusaini mkataba.

Akizungumza na tovuti maalumu ya klabu hiyo, amesema anajisikia furaha kwa sababu maisha yake yake yapo kwenye mazingira salama.

“Najiona mwenye bahati. Nafurahi sana klabu yangu imeniongezea mkataba mwingine.”

“Najivunia kusaini mkataba mrefu kwa sababu nitaendelea kuwepo hapa. Tunapambana tupate mafanikio na nitafanya juu chini kuwapa furaha mashabiki wetu,” amesema.

Chilwell alijiunga na Chelsea akitokea Leicester City kwa kitita cha Pauni 50 milioni akasaini mkataba wa miaka mitano.

Beki huyo wa kimataifa wa England anatambulika kuwa mchezaji muhimu The Blues tangu alipoisaidia kutinga robo fainali ya Ligi Mabingwa Ulaya msimu huu.

Itakumbukwa kwamba Chilwell alikuwa akisumbuliwa na majeraha yaliyomuweka nje ya uwanja kwa muda wa miezi sita baada ya kuboronga katika fainali ya Kombe la Mataifa Ulaya (Euro 2020) akilitumikia chama lake la England.

Awali beki huyo alikuwa katika ubora wake kabla ya kuumia goti.

Mbali na goti, mchezaji huyo alipata maumivu mengine ya misuli yaliyomsababishia kukosa fainali za Kombe la Dunia zilizopofanyika Qatar mwaka jana.

KMC FC yamtimua Hitimana, Julio alamba kazi
Kocha Singida Big Stars amtaja Fiston Mayele